MISHE-BOY

Sport | Hawa ndio warithi wa Paul Pogba na Shaw, Manchester United

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho yupo kwenye mpango wa kukamilisha saini ya kiungo wa Real Madrid  Toni Kroos ambaye anatabiriwa kuondoka  Real Madrid kufikia mwisho wa msimu huu.
 
Kwa mujibu wa gazeti la The Sun imeeleza  kuwa hakuna mahusiano mazuri kati ya Paul Pogba na meneja wake Jose Mourinho. The Sun limegundua kuwa Mourinho na Pogba hawaongei kwa sasa na wakimtumia kocha msaidizi Rui Faria ili afikishe mawasiliano
Bila shaka Metro kutoka Uk limeeleza kuwa Mourinho atahamishia  mipango yake kwa kiungo wa PSG Marco Verrati endapo ataikosa saini ya Tony Kroos ambaye alijiunga na Real Madrid kwa dau la £24 Milioni akitokea Bayern Munich.
Tuwakumbushe kuwa Paul Pogba na Luke Shaw ambaye ni beki wa kushoto wanatabiriwa  kuondoka Manchester United katika kipindi cha majira ya joto, huku Jose Mourinho akijipanga kupeleka ofa ya £45 milioni katika Klabu ya Juventus kumsajili Alex Sandro ambaye atamurudilia Shaw. Pia Mourinho anatazama uwezekano wa kumsajili  Rafael Varane wa Real Madrid huku akiandaa ofa ya £70 milioni kuishawishi Real Madrid.

Hakuna maoni