Sport | Bolt bado atachukua mda ili awe mchezaji mkubwa wa Level ya juu
Peter Stoger Kocha wa Burussa Dortmund amesema kuwa Usain Bolt bado ana mambo mengi ya kufanya ili awe mwanasoka wa level za juu.
Bolt ambaye ni mwanariadha mstaafu akiwa na medali nane za dhahabu
amejiunga kwenye mazoezi ya kikosi cha Borussia Dortmund ili
kutimiza ndoto yake ya kuwa mwanasoka na ajiunge katika klabu ya Manchester United
ambayo anaishabikia.
Kocha tayari ameona kipaji cha soka kwa mwanariadha huyo amekubali kuwa Usain Bolt bado ana safari ndefu katika mchezo wa soka.
kocha huyo alisema kuwa Usain alipewa kipaji ya kucheza ila akitaka kucheza ili awe mwasoka maarufu duniani na kuwa na level za juu bado kazi kwake ingali ndefu kufikia huko.
Kocha aliendelea na kusema kuwa ufiti aliopata kwenye mchezo mwingne ni tofauti na soka huku Stoger akifurahia kukutana na mwanariadha huyo.
Bolt kwasasa anashikilia rekodi ya dunia ya mbio za mita 100 alikuwa pia
kwenye mazoezi ya soka na klabu ya Mamelodi Sundown ya South Afrika
mwezi. January mwaka huu na atashiriki katika mechi ya Matendo ya Huruma
itakayopigwa Old Trafford mwezi June mwaka huu.
Post a Comment