MISHE-BOY

Sport | Sababu ya kukamatwa kwa Saido Berahino na askari polisi huko London

Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, akichezea kwasasa Stoke City, Saido Berahino alikamatwa na askari polisi huko London.

Baada ya kuonekana akitoka nje ya Restaurant-Bar alionekana akiendesha gari lake baada ya mda mchache alionekana akisimamishwa na askari polisi wakimshtumu kwa kosa la kuendesha gari lake kwa kasi akiwa amelewa.

Jumatatu, februari 18, 2019 asubuhi, maheneo ya Great Russel Street palikuwa na sito fahamu pindi polisi walipofika mahali hapo, gari la mchezaji lilionekana kuendeshwa kwa kasi, gari hilo lilisimamishwa haraka na polisi akiwemo Saido pia.

kwa mjibu wa habari Saido berahino alidai kuwa alishambuliwa na kundi kilichozunguka gari lake, na kundi hiyo ilijaribu kuiba funguo za gari lake. kwa bahati nzuri aliweza kuepuka, ndiyo sababu aliendesha gari akikimbia kwa kasi.

Mwishowe aliachiliwa huku akisindikizwa na askari polisi mpaka nyumbani kwake.

Hakuna maoni