Sport | Bumamuru yanuia kumaliza miongoni mwa timu nne bora
Lakini ikiwa bado mapema sana, Kocha mkuu wa timu ya Bumamuru Fc ambayo ilipanda daraja msimuu huu kutoka daraja la pili, Thierry Nimubona amesisitiza kuwa lengo lake ni kuwa miongoni mwa timu nne bora katika ligi kuu Primus League.
Baada ya kupata ushindi wake katika mechi ya kwanza ya ufunguzi wa ligi kuu dhidi ya Rukinzo (2-0) timu ambayo imepanda daraja nayo na zinashiriki zote daraja la kwanza msimu huu, Thiery alisema kwamba ataendelea kuwaambia wachezaji wake kutia bidii ili kumaliza msimuu huu wa soka kati ya nne bora.
Kocha Thierry ameongeza kuwa ushindi wa mabao 2 kwa 0 dhidi ya Rukinzo umewapa matumaini ya kujaribu kukosoa makosa madogo madogo ili wapate matumaini ya kumaliza msimuu huu katika nafasi nzuri.
Post a Comment