MISHE-BOY

Burundi dhidi ya Tanzania hapo tarehe 07/09/2014 mjini Bujumbura

timu ya taifa ya Burundi Intamba Murugamba, ifikapo tarehe 07 mwezi wa tisa mwaka huu saa tisa kamili kwenye uwanja wa mwana mfalme Prince Louis Rwagasore, timu ya Intamba itaipokea timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars nchini Burundi  uku ikiwa ni mchezo wa kirafiki kwa kujiandaa vizuri kwa kombe la CECAFA itakao dhuru nchini Ethiopia mwezi wa 11. kocha ambae anaye ongoza mazowezi ni kocha Rainer WILLFELD akisaidiwa na Massoud IRAMBONA , Etienne, KAZE Cedric , NDIZEYE Jimmy, Dany , Amidou HASSAN  na Vladmir NIYONKURU
wachezaji wamekwisha anza kujiandaa vizuri kwa wale walio itwa na pia wachezaji wanao cheza mpira wakulipwa nje ya nchi kama Saidi NTIBAZONKIZA akiwa nchini Uturuki, Tambwe AMISSI , KWIZERA Pierre  na KAVUMBAGU Didier wakiwa Tanzania.
wachezaji ambao wanazidi kufanya vizuri nje ya nchi ni pamoja na Saidi NTIBAZONKIZA, baada ya kujiunga na klabu ya mpya ambao imemsajili msimu huu; kwenye mechi yake ya kwanza juma pili ilio pita ameweza kufunga goli moja kati ya goli mbili za klabu yake ya Uturuki.
 na Aboul Razak Fiston anazidi kufanya vizuri kwa kufunga magoli katika klabu yake ya Kenya Sofapaka.
tuwafahamishe kuwa ni wachezaji 36 ndio waliitwa na kocha Rainer WILLFELD, wakiwemo wachezaji 4 kutoka nje ya nchi ni pamoja na Saidi NTIBAZONKIZA akiwa nchini Uturuki, Tambwe AMISSI , KWIZERA Pierre  na KAVUMBAGU Didier wakiwa Tanzania, idadi iyo ya wachezaji 36 watapunguzwa na wengine wataongezwa upande wawachezaji wanao cheza nje ya nchi.
 ifikapo tarehe 4/09/2015 ndio timu ya taifa Intamba Murugamba itaingia kambini (locale).

Hakuna maoni