Sport | kauli ya kiongozi wa JS Kabyle kwa Fiston Abdoul Razzak
Timu ya mshambuliaji nyota mrundi Abdoul Razzak Fiston, JS Kabyle ya Algeria ilifanikisha kupata ushindi wao wa pili nyumbani kukamilisha pointi tatu za ushindi dhidi ya USM Bel Abbes (3-1), Jumanne iliyopita katika uwanja wa 1er. Novembre ya Tizi Ouzzou.
Mshambuliaji wa Burundi, Abdoul Razzak Fiston ambaye amejiunga na timu hiyo msimu huu, kwa mchezo wake wa kwanza na Yellow and Green, aliwavutia sana mashabiki wa JSK kwa kufunga mabao mawili pekee yake na kuonesha kiwango kikubwa zaidi.
Aidha mwisho wa mchezo kiongozi wa JD Kabyle, Cherif Mellal alifunguka mbele ya waandishi wa habari na kusema :
"Ninafurahi sana kumwona Fiston akishamiri kwa mara yake ya kwanza katika uwanja huu, hii ni kipengele kikubwa ambacho kitakuwa na faida. Nina maana pia kuwa hakuna nyota katika timu kwa sababu kila mchezaji ana sifa zake, lengo letu ni kugeuka na kuandaa michezo mingine katika hali nzuri kwasababu bado tuna mechi nyingi kubwa mbele."
Post a Comment