Sport | Niya yangu ni Kombe la Raisi tu, Ligi Kuu, LLB ni timu kubwa_ asema kocha YAOUNDÉ
Timu ya Vital'o tayari inaendelea vizuri sana baada ya kumurudisha kocha wake wa zamani, Jean-Gilbert Kanyankore Kagabo al marufu kama Yaoundé akizidi kutamba katika mechi tatu zote bila kupoteza ata moja.
Akizungumza baada ya kutoka sare ya bila bila (0-0) dhidi ya Wabingwa tetezi LLB Machi 07, Jean-Gilbert Kanyankore Kagabo al marufu kama Yaoundé alisema kuwa niya yake ni kuchukua kombe la Raisi na kuendelea kupata matokeo mazuri kwa kila mechi wanayokutana nayo
''unajua kama kikosi ninachho nimekikuta na naendelea kujitaidi kukiweka sawa na baada ya mechi tayari ninaimani kama nitakua na sura nzuri, niya yangu nikuchukua kombe la Raisi najua timu zingali zinawania , nitaendelea kufanya vizuri kwa kila mechi na kuchukua pointi muhimu sio kama nadharau wapizani ila msimuu kwasababu nimeanza na Vital'o kwenye Kombe la Raisi basi kiu changu na ya wanavitalo ni kuchukua kombe hiyi pia wachezaji wangu wapo kwajili ya kupata ushindi'', alisema Yaounde.
Aidha kwanini kocha huyu haweki matumaini ya kuchukua ubingwa wa Ligii Kuu ata kama kila timu kwasasa zinakamilika kufanya vizuri na kuwa bingwa, kocha wa Vital'o alifunguka na kusema
''LLB ni timu kubwa kwasasa kila mtu anafahamu ilo ila kila idara msimu huu imekamilika na kila kitu kinawezekana kwa kila timu zinazo wania Ligii kuu ila endapo ikitokea mimi kuwa Bingwa itakua imebidi tu kwasababu sikuanza na timu ili niiandae kuchukua ubingwa kama kawaida yangu. Nafurahia sana mashabiki waa timu kwa kuonesha upendo wao ninacho kiona ni furaha usoni mwao'', alimalizia kocha Jean-Gilbert Kanyankore Kagabo al marufu kama Yaoundé
Post a Comment