Sport | CAN2019 : Burundi wana Fiston na Gabon wana Aubameyang
Mataifa mawili yatakutana kwa kuwania tiketi ya kufuzu kombe la Afrika CAN2019, Gabon itaipokea Burundi Septemba 08.
Timu ya taifa ya mshambuliaji wa Arsenal ya Uingereza inaonekana kuwa vizuri kwa mtazamo huku Burundi mwaka huu wachezaji wake wengi walikua wakicheza soka nchini hapo walipata soko nje ya nchi huku ikiwa na mchezaji mmoja anayechezea nchini katika orodha iliyojielekeza Ethiopia kwa mechi ya kirafiki atimaye Gabon kwa mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Afrika 2019.
Aubameyang (Mechi 3 bao 1, mimu huu) ambaye yuko miongni mwa washambuliaji hatari wa Afrika nyuma ya Mo Salah wa Misri, lakini vita ya sasa hivi watu wanasubiri atasaidia nini nchi yake wakati kikosi cha Burundi kuna mshambuliaji hatari ambae anaona lango kila mara wa klabu JS Kabylie, Aboul Razzak Fiston (Mechi moja na goli 2 msimu huu).
Watu wanasubiri kuona nyota hawa watasaidiaje nchi zao wakati wanashamiri kwenye klabu zao, upinzani wa Aubameyang na Fiston inaonekana kuwa kubwa zaidi.
Gabon inajipanga vizuri pia Burundi haitakubali kupoteza mchezo wao wakati wana pointi tatu wakiwa mbele ya Gabon katika msimamo wa kundi.
Post a Comment