MISHE-BOY

Burundi: Mwanamuziki wa kike Iry Tina anatarajia kurudi Burundi kwa uzinduzi wa album yake

Mwanamuziki wa kike mrundi mwenye makazi yake Kampala nchini Ouganda, Iry Tina anatarajia kurundi nchini mwake Burundi kwa uzinduzi wa album yake itwayo Kingwera wa.
Iry Tina ni mwanamuziki mrembo kutoka Burundi mwenye makazi yake Kampala na tayari amejijengea sifa nyingi nchini Uganda kwa style yake nzuri na mashahiri ambayo mara kwa mara akiitumia katika nyimbo zake zote uku akipendelea kurikodi nyimbo zake katika studio  Opera Record ya Ouganda.
Baada ya kuka miezi kadhaa ugenini nchini Ouganda, Iry Tina amechukuwa fursa ya kurudi nyumbani Burundi, kwa uzinduzi wa albam yake mpya mwezi wa Julai.
Tuwakumbushe kuwa Machi 12 mwaka huu  2016, mrembo huyo Iry Tina amekuwa  Burundi katika tamasha akishirikiana na msanii wa Ouganda Liane.

Hakuna maoni