MISHE-BOY

Sport | Warundi wa 5 wakutana kwenye fainali nchini Djiboutie

Wachezaji 5, kipa Nzokira Jeff, Ntirwasa Sudi na Manirakiza Haruna (Lucho) wa  A.S.A.S DJIBOUTI TELECOM, kipa Mbonihankuye Innocent Madede 
pamoja na Kaze Gilbert Demunga wa Universite De Djibouti FC,  raia wa Burundi  watakutana kwenye fainali ya Kombe ya Djibouti ( Coupe de Djiboutie) kwa mara ya kwanza kunako michuano ya kombe hiyo timu mbili ambao zina wachezaji kutoka nje wachezaji zaidi ya 5 kukutana kwenye fainali.

A.S.A.S DJIBOUTI TELECOM iliyoondoa timu ya Arta Solar7 kwa mabao 3-0, kwa ushindi huwo timu ya A.S.A.S DJIBOUTI TELECOM imetinga fainali ya kombe hiyo dhidi ya Universite de Djiboutie.

Hii ni mara ya kwanza kwa warundi hawo kukutana katika fainali ya Kombe ya Djibouti, endapo  A.S.A.S DJIBOUTI TELECOM itashinda fainali hiyo basi kipa wa timu ya taifa ya Burundi, Nzokira Jeff  ndiye atakaekuwa mchezaji wa kwanza kutoka Burundi kushiriki na kuchukua mara nyingi kombe hiyo tofauti na wengine wa nne.
Warundi hawo wamejiweka nafasi nzuri ya kucheza fainali hiyo na kuweka rikodi nchini hapa kwa kuzungumziwa sana kama ndio wachezaji wanaozibeba timu hizo kufanya vizuri kwenye michuano zote.

Hakuna maoni