MISHE-BOY

Sport | Patrick Mboma ashanga kuona Seedorf na Kluivert kuwa makocha wa Cameroon

Kwa sasa Clarence Seedorf ndiye kocha mpya wa timu yataifa ya cameroon na atasaidiwa na Patrick Cluivert, kitu ambacho kinamshangaza sana mshmbuliaji wa zamani Cameroon, Patrick Mboma.

Aliulizwa na So Foot juu ya uchaguzi huu, mboma hakuficha mshangao wake. ''Kulikuwa na uvumi,... nilikuwa likizo huko Cameroon, kwa hiyo nilikua najua kuna mawasiliano. Kwa kweli nashangaa. Seedorf ana uzoefu mkubwa sana wa kufundisha, hajawai kukaa katika kazi miezi sita, tangu Ac Milan, Fc Shenzhen au Deportivo la Coruna. hakuwa na matokeo mazuri sana. Alishindwa kuokoa Depor. Kluivert ambaye atakuwa msaidizi wake, alikuwa tu kocha wa Curacao. Bado nina mashaka na hawa makocha.''
''Najua Wengi wako kama mimi! washangaa! wengi walifikiria kuona kocha ambaye anajua au anauzoefu wa Afrika vizuri. Au wa ndani. Mara nyingi ilikuwa vizuri zaidi wachukuwe suala la Rigobert Song, Kocha wa ya ndani. ata jina langu lilitajwa wakati sikuwa mgombea kabisa. Wakati niliulizwa kama naweza kuwania kuwa kocha mkuu, nilijibu hapana. Kama unaishi hapo hapo ni raisi kuelewa mambo mengi ya nchi na wachezaji''.


''Kweli nilishangaa sana mpaka sasa,  na nilijua bila shaka. Sasa waache wafanye kazi ili tuangalie mawazo gani Seedorf na Kluivert wanataka kuanzisha, na wachezaji ambao Cameroon itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Comoros mnamo Septemba. Itakuwa nzuri wa kianza na kushinda. Lakini tutatakiwa kutenda haraka na kuchukua maamzi kwa kuchagua kocha kabla ya mwaka ya michuano, ni hatari. ni hasara sana kuchukua mtu hajawai kufundisha timu yoyote Afrika, ambaye hazungumzi Kifaransa, ingawa najua Kluivert anaongea kidogo kifaransa, inaweza kuleta mshangao. Mimi ni raia wa Cameroon na naitakiya mafanikio timu yangu ya taifa ambayo naipenda sana toka moyoni.


Hakuna maoni