MISHE-BOY

Sport | Inter Star yazidi kutisha katika Usajili

Timu ya Inter Star itakayo shiriki ligi ya daraja ya pili baada ya kuteremka daraja msimu uliyopita, inaendelea kukimarisha kikosi chake kwajili ya kujiandaa na Ligi B msimu huu na kujaribu kuona kama timu itarudi daraja la kwanza.

Uongozi wa timu huyo unaendelea kukimbizana na mda wa usajili uliobakiza kukamilika. Kupitia kwa kiongozi anayeusika na suala la usajili, Tarack amesema bado wanaendelea kufanya usajili kwa ajili ya kutaka kukiimarisha kikosi chao kalba la zoezi hilo kufika mwisho.

Muandishi wa mtandao huu ameshuhudia kiongozi huyo wa timu hiyo akiwatambulisha wachezaji wawili, mshambuliaji Burume Ramadhan Mulamba na kiungo Harerimana Lewis alias Kubi kwa ajili baada ya kusaini mkataba kila mmoja wa mwaka moja.
Hadi sasa Inter Star tayari imeshakamilisha usajili wa wachezaji zaidi ya nane wapya. 

Hakuna maoni