MISHE-BOY

Rukinzo yatamba, Ngozi City haitoki salama Buganda

Timu ya askari polisi nchini Burundi, Rukinzo iliyopanda daraja msimu huu imeweka rikodi yake mpya katika Ligi Kuu Primus League ya kufunga mabao matano daraja la kwanza kwa mara ya kwanza dhidi ya Ngozi City (5-0).

Kocha wa Rukinzo Kocha Rama ameweka wazi kuwa walizitaka pointi tatu kutoka kwa Ngozi City ili kujiondoa miongoni mwa timu hazina pointi kwenye wiki ya tatu.

Huo ni mchezo wa tatu baada ya kuanza vibaya kwa kupoteza mchezo  wao wa kwanza dhidi ya Bumamuru (2-0) na kutoka sare dhidii ya  Atletico Olympic (0-0) mchezo wa pili.

Rukinzo imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 kwa mara ya kwanza baada ya kutoka sare na kufungwa mchezo mmoja  tangu kuanza kwa ligi msimu huu.
Walipata bao lao la kuongoza kupitia mshambuliaji Arsene baadae mvua ya mabao imetiririka kupitia wachezaji Arsene (2), Pascal (1) na Taki ndiye kakamilisha ushindi wa Rukinzo kwa kupachika goli la tano na kuifanya Rukinzo ipate pointi tatu kwenye uwanja wa Buganda mkoani Cibitoke. 

Hakuna maoni