MISHE-BOY

Sport | Dieu-Merci Mbokani arudi Ubelgiji rasmi

Mchezaji wa kimataifa wa Kongo, Dieu-Merci Mbokani baada ya kuwa bila klabu anajiunga na Antwerp kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Baada ya miaka mitano ya kuondoka kwake katika klabu ya Anderlecht, Dieumerci Mbokani anaamua kurudi tena Ubelgiji, mshambuliaji wa kimataifa wa Kongo amesajiliwa kwa msimu moja na Antwerp timu ya kocha Laszlo Boloni.
Akiwa na umri wa miaka 33, ambaye alifanya vizuri na Standard Liege, alikuwa bila klabu tangu mwisho wa mkataba wake na Dynamo Kiev mwezi Juni. Antwerp itakuwa klabu yake ya nane huko Ulaya baada ya kupitia katika klabu kubwa kama Monaco, Norwich au Hull City, ... huku timu yake Afrika aliyochezea  ni Tp Mazembe.


Hakuna maoni