News | Msanii ni lazma atowe pesa ili apate promotion asema Christian Bella
Hii swala imekuwa ngumzo sana nchini Burundi upande wa wasanii wanadai kwamba, media (watangazaji) inachangia kwa kiasi kikubwa muziki wa Buja fleva kutokuendelea kama nchi zingine za Afrika Mashariki. Agosti, 17, 2017, Christian Bella msanii wa Bongo Fleva alifunguka mbele ya waandishi wa habari na kusema,
''Nilifanya wimbo na msanii wa Burundi, Daddy Face aliniambia anataka kuja Tanzania na anapendelea wimbo wake upelekwe kwenye TV, Radio, nikamuambia hapa nchini kwetu ukitaka promo lazma utengeneze bageti kubwa (pesa). Ata sisi huko Tanzania ata uwe na jina kubwa kiasi gani, hauwezi kupeleka wimbo wako redioni au TV na kuwaambia mchukuwe mupige, uongo hasikudanganyi mtu. Sisi tunafanya show tunapata pesa, yeye (mtangazaji) anakaa ana ku play na anakuongelea inakubidi mpe ata maji, kwakuwa sisi tunafaidika tunapata pesa kwenye show kupitia yeye (mtangazaji), kwanini husimpi pesa?, narudi kusema tena sisi tuna njaa sana (wa Bongo) bado hatujaridhika ndio kwa maana tunaendelea kutumika ili tuendelee kupata.''
Post a Comment