News | Wasanii wa Bongo Fleva ni wa maskini sana kuliko wa Buja Fleva
Ninaimani unaweza ukapatwa na mshangao kwa kile ambacho nimetanguliza mwanzo kwa kusema kama wasanii wa Bongo Fleva wana njaa sana kuliko wa Buja Fleva au Burundi Fleva kwa ujumla.
Ukubaliane nami kwamba ni ukweli ninacho kiongea hapa na kitu hichi nilikua nakifikiria sana tangu zamani mpaka leo msanii moja kutoka Tanzania kathibitisha aya mbele ya waandishi wa habari.
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva mwenye asili ya Jamuhuru ya Kidemokrasia ya Congo, Christian Bella alifunguka mbele ya waandishi wa habari katika mahojiano iliofanyika Club du lac Tanganyika nchini Burundi, Agosti, 17, 2018.
Bella alishangazwa sana kuona wasanii wa Burundi ambao walipangwa kuimba nawo kwenye show ya Agosti 18(Tazama cover hapo juu) hawakujitokeza kwenye Press conferenc wakati ndio wenyeji.
''Tukiongelea Tanzania, tunaeshimu sana Media, tuna njaa sana, sisi tuna njaa, hatujaridhika na sisi tunaona media kama ndio ma boss wetu. Tanzania watangazaji tunawaona kama ma boss wetu kwasababu bila nyie habari zetu haziwezi kuwafikia wananchi. Tumetoka mbali tumekuja lazma tueshimu media, nafikir wasanii tunatarajia kupaform nawo kila mmoja alifanya mkataba, hakuna atakae fanya show ya bure. labda Burundi muna system zenu ila wangetuonesha sisi mfano, wao ndio wangepashwa kukaa hapa mbele (Fizzo na Natacha). Labda wana sababu zao ya kutojitokeza hapa ila wanafanya makosa sana inabidi wajikosowe, sisi Tanzania tunakuaga na tabia ya kufika mapema ya media kwajili tunaeshimu sana media kama hawaeshimu media hawatafika popote. Sisi (Bella na Snura) tunaomba hisiwi kesi labda ni style ya Burundi.''
'' Burundi miziki bado haijakolea ila kitu kikubwa mujaribu kuwashauri wasanii wa Burundi wajitume waache uvivu labda sijuwi style ya huku ila naomba hisiwi kesi'', alimalizia Christian Bella.
Licha ya wasanii wa Tanzania kuonekana kuwa wana pesa nyingi kuliko wasanii wa Burundi, Christian Bella alizungumzia hapa kazi, kwasababu msanii huyu tayari amekwisha itembelea Burundi zaidi ya mara 2 na tayari alifanya utafiti na kugundua kwamba wasanii wa Burundi ni matajiri ndio moja ya sababu awataki kujiendeleza kimuziki ili muziki wao utapasuwe kama bongo fleva. Hakika mwenye njaa ndie mtafutaji wa riski licha ya pesa na mafanikio nyingi, wa bongo bado wanaendelea kutafuta na kujituma kimuziki na kwasasa wasanii wao wanaishi kimuziki tofauti na Burundi.
Post a Comment