MISHE-BOY

Sport | Nahimana Jonathan Milenge aibuka kidedea mchezaji bora wa April 2018 nchini Burundi

Baada ya mchakato uliodumu kwa mda mfupi wa mwezi umoja wa April, hatimaye golikipa namba moja wa Vital'o FC na wa timu ya taifa ya Burundi, Jonathan Nahimana Milenge ametangazwa kuwa mchezaji Bora wa mwezi April katika  Ligi kuu Primus League 2018.

Bila shaka ile kauli niliwai kuandika kuwa kwa mtazamo wa karibu endapo golikipa wa Vitalo ataendelea kushamiri bila shaka ataibuka kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu. Ishara inaanza kudhiririka golikipa huyu ameanza kutimiza ndoto zake.

Msimu huu Jonathan amekuwa  akiibeba Vital'o ambapo hadi sasa aliweka rikodi ya michezo 9 mfululizo bila kufungwa ata goli moja huku akiisaidia timu yake kuendelea kuwa bora zaidi katika michuano ya Ligi Kuu na Kombe la Raisi.

Kura zilizopigwa zimetosha kumpa tuzo Jonathan Nahimana mbele ya wachezaji wengine nyota akiwemo mshambuliaji hatari wa Aigle Noir, Shaka Bienvenu pamoja na Dany Cedrick Urasenga maarufu Kagabo.

1. Jonathan Nahimana Milenge : 34%
2. Shaka Bienvenu : 32,8%
3. Dany Cedrick Urasenga  : 32,7%

Hakuna maoni