sport | ASAS Telecom ya wachezaji warundi wa tatu yaingia hatua ya makundi Ligi Arabe
ASAS Telecom ya Djibouti wamefanikiwa kushinda muzunguuko wa awali na kufuzu kuingia hatua ya makundi ya Ligue Arabe, itacheza michuano hiyi rasmi tarehe 17- hadi 24 Mei huko Jeddah.
Goli kipa Nzokira Jeff, Sudi Ntirwasa na Manirakiza Haruna maarufu Luco kutoka Burundi waisadia sana ASAS Telecom kufanya vizuri katika mchezo dhidi Ganz Sport ya Morocco kwa kuishinda bao 3-1, kwa ushindi huwo ASAS Telecom ya Djiboutie imefuzu hatua ya makundi ya Ligi kubwa (Ligue Arabe).
Pointi nne tu imetosha timu hiyi kuingia katika michuano ya Ligue Arabe katika kundii B ambapo itakabiliana na Ittihad Alexandria (Misri), Al-Salmiya (Kuwait) na Fath Union Sport (Morocco).
Kundi nyingine linajumuisha Al-Nejmeh (Lebanoni), ASAC Concorde (Mauritania), Al-Faisaly (Saudi Arabia) na Club Africain (Tunisia).
Tukumbuke kuwa washindi wawili wa michezo hii watajiunga na timu zingine 30 ambazo tayari zinajumuisha mzunguuko wa kwanza wa msimu wa 2018.
Ratiba imepangwa ifuatavyo :
Post a Comment