MISHE-BOY

Sport | Arda Turan asimamishwa mechi 16 za Ligi Kuu nchini Uturuki

Mchezaji wa zamani wa barcelona ya Hispania, Arda Turan alitolewa nje ya uwanja baada ya kumshambulia mwamuzi msaidizi Ijumaa iliyopita, baada ya kuchunguza kwa ukaribu zaidi shirikisho la soka nchini Uturuki imetoa adhabu kwa kusimamsisha mechi kumi na sita (16).

Aidha ni hasara kubwa kwa Arda Turan, kiungo wa Istanbul Basaksehir pia wa timu ya taifa ya Uturuki alipewa kadi nyekundu wakati ameacha mechi kati ya timu yake na Sivasspor (1-1).

Arda Turan alijiunga na istanbul kwa mkopo, alimfuata mwamuzi msaidizi na kumsukuma ndio kosa iliyomsababishia kupata kadi nyekundu moja kwa moja.
Alhamisi hii, Shirikisho la Kituruki limeamua kumpa adhabu ya mechi kumi na sita (kumi kwa kumsukuma mwamuzi, tatu kwa kumtukana na tatu kwa kutoa vitisho dhidi yake).

Itakumbukwa kuwa Arda Turan atapigwa faini ya Liras 39.000 pesa za Uturuki sawa na Euro 7.700.

Hakuna maoni