MISHE-BOY

Sport | Barcelona itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mamelodi Sundowns Mei 16

FC Barcelona itakabiliana na Mamelodi Sundowns, wabingwa wa Afrika Kusini 2018, katika mechi ya kirafiki Mei 16 katika uwanja wa FNB ambayo ilijulikana kama Soccer City huko Johannesburg (saa 16:15 GMT).
FC Barcelona Bingwa wa Hispania watakutana na mabingwa wa Afrika Kusini Mamelodi Sundowns katika mechi ya kirafiki, Mechi hii ambayo inasubiriwa na wengi nchini Afrika Kusini itafanyika Mei 16 kwa kusherekea miaka karne ya kuzaliwa kwa Nelson Mandela, Barcelona ilithibitisha alhamisi hii.

Katika uwanja huwo itawakumbusha wapenzi wa soka kwa mchezaji Andres Iniesta kwasababu ni katika nchi hiyo aliweza kuifungia bao la ushindi nchi yake ya Hispania katika  fainali ya Kombe la Dunia 2010.

Hakuna maoni