MISHE-BOY

Amissi Tambwe anaanza kuwatishia ma klabu pinzani na akimsifu kocha wake wa mpya


Mchezaji tena mshambuliaji hatari sana wa timu ya taifa Intamba Murugamba, Amissi Tambwe, ambae amesajiliwa na Yanga katika dirisha dogo la usajili akitokea Simba, akizungumzia ujio wake na wa kocha Mkuu wa Yanga, Hans Pluijm, kwamba anafurahishwa ujio wa kocha huyo ndani ya Yanga ambapo kikubwa kilichomvutia ni aina ya mazoezi ambayo hajawahi kukutana nayo katika kipindi kirefu cha kucheza soka pamoja na aina ya wachezaji.
 Kocha  Mkuu wa Yanga, Hans Pluijm, anafanya siku chache sana tangu aanze kukinoa kikosi hicho,
Amissi Tambwe, ametamka kwamba huyu ndiye kocha aliyekuwa anamuhitaji katika maisha yake ya soka.Tambwe alisema mazoezi ya raia huyo wa Uholanzi yamejaa ufundi zaidi ambapo kila zoezi analotoa ingawa ni gumu, lakini lina uhusiano wa moja kwa moja kuweza kuwakabili wapinzani wao uwanjani jambo ambalo limemshangaza na ameongeza akisema tena mara amekuwa akikutana na makocha ambao wamekuwa wakitoa mazoezi ya mbio za kutosha hali ambayo imekuwa ikiwachosha wachezaji huku mazoezi ya mbinu yakipungua ambapo sasa anataka kuyashika vizuri mazoezi hayo ya Pluijm kuweza kuwakomesha wapinzani na kurudi katika fomu yake ya kupachika mabao.
 hii maneno imewatia hofu sana ma klabu pinzani ususana klabu yake ya zamani ya Simba ambao imemtowa na kudai kwamba Amissi tambwe amekwisha.
 Alipo ulizwa tena kuusu ujio wa kocha mwenye uraia wa Uholanzi amekuwa na mengi sana ya kumpongeza kocha uyo na uku akiwa na uoga ndani yake, amesema kwamba: “Kiukweli nafurahia sana ujio wa huyu kocha wakati anafika nilikuwa naogopa, unajua kila kocha mpya anapokuja mambo hubadilisha mambo, lakini huyu kocha (Pluijm) ni fundi sana mazoezi yake ni magumu wakati mnayaanza, lakini ni yale ambayo mtayatumia katika mech.
 Tanzania wanafikiri kwamba Tambwe ambae ni mrundi ana nafasi kwenye timu ya taifa ya Burundi ila shirikisho la soka la hapa ndio linajua umuhimu wake kwenye kikosi cha taifa ata kama amekosa mechi nyingi za kwanza za msimu huu akiwa na Simba.

Hakuna maoni