MISHE-BOY

imani moja tutafika mbali na kuonekana vigogo na kutisha ki soka kama ma timu zinginezo


ni jambo nzuri na ya kupongeza sana kuona mabadiliko inaanza kuja kwenye soka ya Burundi. ni myaka nyingi sana Timu ya taifa ya Intamba ilikua aina uzowefu wakucheza machi ya kujipima nguvu na baadhi ya timu za nje. ila kwa uongozi wa Mheshimiwa Révérien anazidi kujituma na kuonesha kujali sana maendeleo ya soka izidi kuendelea mbele na tuwe na sura nzuri kwenye orodha ya FIFA  ya ma timu ao klabu zinazo fanya vizuri siku jijazo.
tuki linganisha ziara ya kiongozi wa zamani wa mpira ya hapa nchini Burundi na ya sasa ipo tofauti sana, ziara ya Mama Lydia Nsekera ilikua ya kwenda kuonana na kiongozi wa Soka ya Fifa na bila kuleta mabadiliko yoyote kwenye Timu ya Taifa. ila kamati ya Sasa ya Mheshimiwa Révérien inazidi kuonesha Mabadiliko bali ya kwenda ziarani kuuza sura ila ni yakuwaredjesha wachezaji warundi wanao ishi nje Ya Burundi.
mchezaji Mrundi anaye ichezea klabu ya Newcastle ya Ungereza ligi kuu ya Premier league, amesema kwamba unapokua ugenini kama nyumbani kwenu awakujali inakubidi ujitafutiye mahali pengine ambapo wataona mafaa yako, mi siwezi kujiita kwenye timu ya taifa ila nchi ndio ndio inaitaji kuniita.
basi wakati umefika na Mheshimiwa Révérien yupo ziarani Ulaya na lengo lake sio kwenda kuona Ulaya na kuuza sura, lengo lake nikuwasikilizisha wachezaji warundi wanao chezea nje ya nchi kuwa tunaitaji nchi yetu icheze kombe ya kimataifa ya Afrika 2015, usishangae kuona Ivory Cost iko juu kwa sasa nikwajili ya wachezaji wao kuwa nje ya nchi na unapo cheza mpira wakulipa unakuaga na uzowefu mkubwa sana kuzidi na yule anayecheza nyumbani.
wito kubwa sana Mheheshimiwa ametangaza kuwa kila mtu azidi kuleta mchango wake sio kipesa tu na kimawazo ili tu tuakikishe tumefika ambapo tunaitaji kufika.
amekua namazungumzo na wachezaji wa 2 wanao chezea ligi kuu ya Ungereza, Bigirimana Gael wa Newscastle na Saido Berahino, mazungumzo inaonekana kwamba wameitika kusaidia nchi yao ili ishiriki kwa mara ya kwanza Kombe yakimataifa barani Afrika, kama gisi vijana wetu walivyofanya vizuri kufikisha timu ya Intamba kwenye Kombe ya Chan kwa mara ya kwanza. kila kitu kinawezekana ila ni kwa pamoja ya kila mrundi ambae anaye ipenda nchi yake, hii ni msemo wake Berahino Saido.
hivi ukitizama wachezaji wengi wa Burundi wanacheza mpira wa kulipa nje ya nchi kama Ntibanzonkiza Saidi, Valery, Demunga, Cedrick, Tambwe, Papy Faty, Ferre, Lucio, Selemani, Pierrot, Kadogo, Steve, Gael, Berahino, ukitizama listi nzima ni wa pro tu na kwa pamoja iyo kweli tutafika mbali sana ambapo kila Mrundi anaitaji kufika.
hii ndio mpangilio wa Kombe ya Afrika 2015 nchini Maroc, ni kwamba kombe itaanza mwezi wa kwanza January tarehe 17/2015 mpaka tarehe 7/2015, mechi za mtuano  ya awali itakua ni tarehe 11-12-13 avril 2014 (aller) na 18-19-20 avril (retour).
kura  ajili ya mzunguko wa pili na hatua ya makundi utafanyika Aprili 27, 2014 mjini Cairo.

 HABARI NZURI NIkwa upande wa ligi ya mabingwa  barani Afrika ambapo klabu ya hapa Burundi Flambeau de l'Est imejielekeza nchini cameroun ili kuchuana dhidi ya klabu Cotton Sport de Garoua baada ya kuiondoa Klabu ya Congo Brazaville les Diables Noirs,  na ivi inaendela kufanya vizuri kwa kupata ushindi ugenini kwa bao 1-0.
Flambeau de L'Est
 tuwakumbushe kuwa mechi ya Intamba dhidi ya Rwanda Amavubi ni hapo tarehe tano, njooni kwa wingi kuispoti timu ya taifa kwa njia zote na hali, kasi zote, vijana wetu wajiisi kama wanajaliwa na wanainchi wao.
 
 habari njema nyingine ni kwa wachezaji wetu warundi wa wili wanao cheza Djibouti Andosango Freddy na Nzokira Jeff( kipa wazamani wa vital'o na wa timu ya taifa Intamba).
Nzokira Jeff  & Andosango Freddy
 jana tarehe moja mwezi wa tatu ndipo walicheza mechi yao kwenye klabu yao ya A.SAS Djibouti Telecom na kupata ushindi wa mabao 2-1, kupelekea ushindi wao wa jana na mechi kati ya A.S PORT na GARDE REPUBLICAINE kugawa pointi.  tukumbuke kuwa wapinzani wao ni hii klabu ya  GARDE REPUBLICAINE, imepoteza izo pointi 2 dhidi ya AS Port na ikapelekea klabu ya wachezaji warundi ya  A.SAS Djibouti Telecom kutawazwa washindi wa ligi kuu ya Djibouti kwa mara ya pili mfululizo.  kunabaki mechi tatu mbele ya kumalizia ligi ata wapigwe mechi zote zilizo saliya ni washindi tu.
Nzokira Jeff
mwaka wake wa kwanza alipo jiunga na hii klabu yake, mchezaji Nzokira Jeff amechaguliwa kama Goli kipa wa kwanza kwakufanya vizuri zaidi ya wengine(meilleur gardien), na kwa huu mwaka yupo na imani yakutawazwa tena na kupata zawadi nzuri.

habari ya uzuni kidogo ni kutoka kwake mchezaji Kaze Gilbert Demunga anaye ichezea klabu ya simba Ya Tanzania, ni mgonjwa wa goti lake na anamechi kama 2 za ligii kuu ya Tanzania achezi kwajili ya madhara inayo mkabili kwenye mguu wake.n iyo inaonesha kwamba tutaweza kumukosa kwenye pambano ya Intamba vs Amavumbi hapo tarehe 5. endapo atajisikia yupo safi wataweza kumuweka kwenye mechi ila ukweli ni kwamba anaumwa.
Kaze Gilbert



Hakuna maoni