Sport | Saido Berahino mchezo wake wa kwanza na Burundi afunga bao
Mshambuliaji aliyepewa nafasi katika kikosi cha England na kocha Roy Hodgson kwa mechi ya kuwania kufuzu Euro 2016 dhidi ya Slovenia, Saido Berahino aliamuwa kuichezea nchi yake ya taifa Burundi mwaka huu wa 2018 na mechi yake ya kwanza Jumamosi hii dhidi ya Gabon aliweza kupachika bao lake la kwanza katika mchezo wake wa kwanza.
Nyota wa Stoke City, alihitaji tu dakika 40 kuweka rikodi ya kipekee jijini LibreVille katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Afrika 2019 .
Tuwakumbushe kwamba Burundi haijawahi kushiriki katika Kombe la Mataifa la Afrika, lakini kwa fursa hii inaweza kutimiza ndoto zao kwa kuwa mwaka huu wanawachezaji wengi wazuri wanao cheza nje ya nchi.
Post a Comment