Sport | Aubameyang anaiokoa Gabon dhidi ya Burundi
Timu ya taifa ya Gabon inaendelea kupoteza mchezo baada ya kupigwa na Mali (2-1) katika mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu Kombe la Afrika can2019, walishindwa kujitetea kwa mara ya pili wakiwa nyumbani dhidi ya Burundi (1-1).
Vijana wa José Antonio Camacho walikubali kupigwa bao la kwanza iliyowekwa wavuni na mchezaji wa zamani wa Uingereza Saido Berahino ambaye alikuwa akiadhimisha mechi yake ya kwanza na Intamba Murugamba (39').
Mchezaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang, aliifanya jitihada yote na kuokoa timu yake kwa kusawazisha (74').
Gabon inatimiza pointi 1, Burundi pointi 4 wakati Mali ambayo itajielekeza Jumapili Sudan ya Kusini bado ina pointi 3 na Sudan ya Kusini haina ata pointi.
Post a Comment