MISHE-BOY

Sport | Gabon watamkosa Denis Bouanga dhidi ya Burundi

Habari mbaya  kwa timu ya taifa ya Gabon ambayo itakutana na Burundi katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Afrika CAN2019. Denis Bouanga aliitwa na Gabon lakini hatakuwepo.

Kwa mjibu wa wa gazeti la Midi Libre, kiungo wa Nîmes alivunjika mkono wake Jumatatu alasiri baada ya kuanguka vibaya. Vyombo vya habari vya Ufaransa vinasema kuwa Bouanga atafanyiwa upasuaji siku ya Ijumaa au Jumatatu na hapasiwi kucheza baada ya mwezi.

Aliwasili Nîmes msimu huu akitokea Lorient, Denis Bouanga tayari amewai kuichezea timu yake ya taifa Gabon mara 8. Ndie kiungo anaelewana sana na mshambuliaji wa Arsenal, Aubameyang kwa uchezaji.

Hakuna maoni