MISHE-BOY

Sport | Vital'o Fc yapigwa tena, Kocha bado ana kazi kubwa

Timu ya Vital'o imekubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Flambeau de L'Est katika mchezo wa Ligi Kuu Primus League nchini Burundi uliyofanyika uwanja wa mkoani Gitega.

Vital'o ni timu itakayowakilisha Burundi katika michuano ya Kombe la Shirikisho kwa matokeo aya ata kiwango cha wachezaji bado matumaini ya kufanya vizuri itachukua mda mkubwa.
Kipigo hicho ni cha pili kwa vijana wa Kanyakore hao kufuatia kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Aigle Noir katika mchezo wa kwanza wikiende iliyopita.

Kocha mkuu wa timu hiyi, Gilbert Yaoundé Kanyakore anaonekana bado ana kazi kubwa ya kufanya mazowea kati ya wachezaji hawo ambao timu nzima ni wachezaji wapya.

Katika wiki ya pili Vital'o ipo nafasi ya 15 kwenye msimamo ikiwa haina ata pointi na goli wakati Aigle Noir na Musongati ndio timu pekee ziko kileleni na pointi sita kila mmoja.

Hakuna maoni