MISHE-BOY

Sport | Musongati yawaka na kuonekana bora zaidi

Tunapo zungumzia kuwaka mota ni kama gari limewaka moto, Musongati imeanza kuonekana bora katika michezo ya kirafiki na wengine kuanza kuitabiria ubingwa msimu huu ila bado mapema sana.

Baada ya kuwachapa Olympic Star mabao 4-1 katika mchezo mkali kabisa uliyofanyika wikiende iliyopita huko mkoani Gitega na Messager Bujumbura wiki ya pili ilikumbana na kipigo cha mabao 2-1.

Ikiwa ugenini mkoani Rumonge, Musongati ilizidi kuwa imara na kumiliki mpira kuliko wenyeji Messager Bujumbura, mabao ya Musongati yalifungwa na mchezaji wa zamani wa Vital'o, Joseph Kashindi maarufu Jeph Bakis na Pascal.

Kwasasa vijana wa kocha Hussein Wello wanaongoza baada ya kushinda mechi zao zote mbili ilizocheza hadi sasa. 

Hakuna maoni