Sport | Timu mpya ya Zinedine Zidane yatambulika
Kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane amekwisha pata klabu mpya ijayo. Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa anatarajia kujiunga na Juventus kuchukua nafasi ya Massimo Allegri.
Tangu wiki kadhaa, bingwa wa dunia wa 1998 ametangazwa kujiunga na Manchester United kuchukua nafasi ya Jose Mourinho, lakini kuna uwezekano mkubwa wa kocha akajielekeza nchini Italia siku zijazo.
Kulingana na gazeti la El Mundo, Zinedine Zidane anatarajia kukaa benchi ya Juventus mwishoni mwa msimu wa sasa. Gazeti hiyo ya Ispania inaendelea kutangaza kila siku kwamba viongozi wa Juventus tayari walikamilisha mpango wao pale ambapo walimaliza uhamisho wa Cristiano Ronaldo msimu huu na itaendelea kukamilisha mpango wa kocha mfaransa.
Post a Comment