MISHE-BOY

News | Melyna Mshindi kuachia wimbo 'How Much' Jumatano

Muimbaji wa kike wa nyimbo za Injili kutoka Burundi, Melyna Mshindi amesema kuwa anatarajia kuachia nyimbo yake mpya inayoitwa kwa jina la ''How Much'' siku ya Jumatano.

Ni muda mrefu mwana dada huyo amekuwa kimya lakini kwa sasa ameonekana kuanza kuachia kazi zake kwa kasi ikiwa tangu alipoachia wimbo wake wa kwanza ''Feel Beta'' aliyomshirikisha GNL FLS.

Melyna anatokea katika familia ya muziki ikiwa kaka zake wote wawili ni wanamuziki (Prince Mshindi na Floris) na tayari amekwisha shirikishwa katika nyimbo na wasanii wakubwa wa gospel nchini hapo, Hervé, Norasque, Big Zoé pamoja na GN.

Hakuna maoni