MISHE-BOY

News | Hakuna wimbo wa Sat B iliyotoka ikagoma kuwa hit


Uzuri wa muziki ni vyombo, sauti na melody lyrics sio sana. Ndio maana Fally Ipupa anazidi kuiteka Afrika hata dunia nzima na kilugha tusiojua lingala ila ni vyombo, melody na sauti yake.

Kwa utafiti wa karibu, hakuna msanii kama Sat B kwenye muziki wa Bujafleva, kinacho baki ni msanii mwenyewe kutazama na kuelewa kama nyumbani amekwisha maliza kinacho fuata ni  yeye kutangaza muziki wake kimataifa ili tasnia ya muziki  nchini hapo ijivunie jina lake kwenye muziki.

Mashabiki wengi wamekuwa wakijiuliza kuhusu lini muimbaji Staa wa Bujafleva atatoa wimbo mpya mpaka na wengine kuamua kuvujisha wimbo wa msanii huyo 'GirlFreind'' aliyomshirikisha Dully wa Bongo Fleva. 

Sat B ni msanii pekee wa Burundi hajawai kutengeneza wimbo ikagoma kuwa hit, hata mashabiki ni mashahidi kwa mfano tumeona Too Much, Ivyo Bintu, Feel Love wakati hiyi bado inaendelea kufanya vizuri huku kuna mpya ''No Love'' inayozimisha nyimbo nyingi nchini hapo.

Hakuna maoni