MISHE-BOY

News | Lolilo amini kuwa wasanii wanamuroga ndio sababu kafanya ajali leo


Msanii wa muziki wa Buja Fleva, Lolilo maarufu Lizzo Mzizi wa Jiwe au Simba alifanya ajali ya gari leo Agosti 13, 2018 akitokea kudumbuiza mkoani Gitega ambapo inatarifiwa kuwa watu walijitokeza kwa wingi kwenye show hiyo.

Licha ya kufanya ajali hiyo Lolilo alisema na kuamini kwamba ajali hiyo bila shaka kuna mkono wa wasanii wanaojaribu kumuroga na kuongeza kuwa wasanii wanarogana ili mmoja afeli wengine waendelee.

Ukijaribu kulinganisha Lolilo wa kipindi kile na wasasa kuna utofauti kubwa licha ya kuachia kazi nzuri ndio moja ya sababu ya yeye kuamini na akihusisha imani za kishirikina na kusema kwamba kamwe hawata muweza kwajili ana mwamini Mwenyezi Mungu.

"Yap nilifanya Show kubwa Gitega watu walikua kibao na wakati narudi Bujumbura nimefanya accident (ajali) gari langu limearibika na najua kwanini yametokea haya wasanii wenzagu wanafanya jinsi yote nianguke kimuziki, nihaibike, nife ila yote bure hawataniweza kwasababu niko pamoja na Mungu, chochote kile watakacho kifanya waambie warozi wao waongezee hawata niweza niko pamoja na Mungu na Mungu yuko pamoja nami", Alisema Lolilo






Hakuna maoni