Newz | R Nawz awataka radhi mashabiki wake
Mwanamuziki wa Buja Fleva anayefanya vizuri hivi sasa R-Nawz amefunguka na kuwataka radhi mashabiki zake wote kwa ile ahadi ya kuachia video ya nyimbo yake mpya ''I Love Mama Afrika'' mwanzoni mwa mwezi February.
R-Nawz aliomba radhi baada ya kushindwa kutimiza ahadi na kudai kupatwa na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake alipo kutana na director na kumuambia gharama kubwa zaidi na hivyo kupelekea kushindwa kutimiza ahadi.
Mwanamuziki huyu ambae kwasasa anatamba na wimbo wake ''Rudi'' aliambia Hot Mishe Mishe kwa kuonesha kusikitishwa kwa kushindwa kuwatimizia mashabiki wake ahadi na kusema
'' Ninamatumaini kila mmoja amekua na wakati mzuri wakutaka kuona kwa mara ya kwanza video yangu, ila nachukua nafasi hii kuwaomba radhi kwakushindwa kuwatimizia. Mbali na hayo nyimbo yangu na kadri nilivyoimba, inaweza ikanigharimu milioni tano ili nikamilishe video nzuri uku uwezo wangu bado ungali wa chini na sina mdhamini ndio moja ya sababu ya mimi kushindwa kutimiza ahadi hata hivi karibuni Mungu akijaalia ntawapa taarifa nzuri kuhusu kazi zangu.''
Post a Comment