MISHE-BOY

Sport | As Vita Club yaangukia katika kundi la kifo


Shirikisho la Soka la Afrika ilifanya hatua  ya makundi ya Kombe la CAF  jumamosi hii katika makao makuu yake huko Cairo .

As Vita Club ya DR Congo iliangukia kwenye kundi ya kifo ambapo itahakikisha inafanya vizuri dhidi ya ASEC Mimosas na Raja Casablanca, pamoja na Aduana Stars.

Willamsville na Djoliba iko katika kundi moja moja na Enyimba pamoja na  CARA Brazzaville.

Upande mwingine wabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Yanga Africans wameangukia kwenye kundi D, ndani ya kundi hilo Yanga Africans watakutana na timu mbili kutoka ukanda wa afrika Mashariki ikiwa ni Gor Mahia ya kenya na Rayon Sport ya Rwanda.

Tazama jinsi droo ya hatua ya makundi ilivyofanyika


Hakuna maoni