Sport | Zaidi ya watu milioni moja wamtaka Mohamed salah kuwa Raisi wa Misri!
Zaidi ya watu milioni moja walipiga kura kwa Mohamed Salah wakati wa uchaguzi wa Urais hivi karibuni wa Misri!
Shujaa wa Liverpool anazidi kuwa nyota wa timu hiyo baada ya kuvunja rikodi kwa kufunga magoli na kutoa pasi za uhakika katika Ligi kuu, pia Salah alisababishia Misri kufuzu Kombe la Dunia 2018, baada ya kupata penalti dakika za mwisho dhidi ya Kongo.
Mohamed Salah tayari kwa nchi yake amekwisha funga mabao 33 katika mechi 55.
Wamisri wa eneo hilo walitumia njia ya kumshkuru Salah kwa kusema asante, walimchagua wakati wa uchaguzi wa hivi karibuni wa rais!
Kwa mjibu wa taarifa za The Economist, wamisri zaidi ya milioni moja walipoteza karatasi zao za kura na baadhi yao walikataa kuwachagua wagombea wawili wa uchaguzi na kuamua kupiga kura kwa Salah.
Post a Comment