MISHE-BOY

Sport | Nategemea kuchukua Kombe la Raisi kwa hali hii_ Vivier Bahati

Mkufunzi wa klabu ya Musongati ya mkoani Gitega inayocheza ligi kuu Primus League, Vivier Bahati alisema kuwa kwasasa hana mpango wakuchukua ubingwa ila nguvu zote anaziweka katika Kombe la Raisi.

Musongati imekua imara kila idara miaka za nyuma na kupelekea moja ya timu ngumu kufungika tofauti na msimu huu.
Hali inazidi kubadilika kiasi kikubwa kwenye klabu ya Musongati mpaka wakata tamaa ya kuwa bingwa msimu huu na kutegemea Kombe la Raisi ambayo watachuana na Atletico Olympic.

Kocha Vivier Bahati alifunguka na kusema, ''hakuna tatizo kwenye timu ila tu tumeanza vibaya  tokea mwanzo wa Ligi ili timu iwe imara na kutafuta ubingwa inabidi maandalizi mazuri mwanzoni na hii hali kwenye soka ni kawaida.
Sijuwi kama msimu ujao kama timu inaweza kurudisha sifa zake kama awali kwasababu sijajuwa viongozi wa  timu wataanda timu kivipi kwajili naweza kuendelea au nikaondolewa haya yote ukiwa kwenye kazi kama hizi zetu ni kawaida ndio moja ya sababu siwezi kusema ya kesho''.

Kocha Vivier Bahati anaungwa mkono na mashabiki wote wa Musongati kwasababu anazidi kufanya kazi kubwa kwenye klabu hiyo uku wengine wakifiri labda msimu huu kuna usiano mbaya na mashabiki ila kocha huyu alimalizia na kusema, '' hahahahaha hahaha mimi sijawahi kuwa na mausiano mabaya na mashabiki wa timu tangu nituwe hapa.''

Hakuna maoni