MISHE-BOY

Sport| Intamba Murugamba U17 yapata mdhamini mpya

Timu ya taifa Intamba murugamba ( Burundi) imepata mdhamini mpya baada ya kuwa na udhamini wa Lumitl kwa miaka kadhaa, kwasasa nyingine imejitokeza hivi karibuni.

Lumitel imekuwa mdhamini mkuu  wa timu ya taifa kwa miaka kadhaa na pia inaendelea kudhamini Burundi mpaka sasa, sasa mdhamini mpya atakuwa kampuni ya  Maziwa, NATURA kutoka nchini Burundi.

Kampuni hiyi itaanza kwa kudhamini timu ya taifa kwenye michuano ya Kombe ya  CECAFA U17  mwaka 2018 ambayo itaandaliwa nchini Burundi.
Kiongzi wa Shirikisho la soka nchini, Mh. Reverien ndikuriyo amefuraishwa sana na kampuni ya Natura kujitokeza kwa kuonesha  upendo wao na kuanza kudhamini timu ya taifa ya watoto wasiozidi miaka 17 na kuomba Kampuni zingine kujitokeza kwa sana kudhamini Timu ya Taifa na Ligi Kuu kwa pamoja ili vijana waweza kuiwakilisha nchi kimatifa wakiwa stamina.

Thamani ya mkataba huo haijafichuliwa.

Hakuna maoni