|
Sat-b |
Baada ya mtoto wa Sat-B kupewa sumu na watu ambao awajulikani mpaka sasa. hapo tarehe 16/02/2015 tumepata habari ya kwamba mwanamuziki Sat-B amepatwa na ajali akiwa kwenye moto uku akiumia sana na amepelekwa Hospitalini. kwa sasa hali ya mwanamziki Sat-B Satura amabafle ni nzuri kabisa ila jicho lake sehemu ya pembeni ya jicho ndo amechanika. Kwamjibu wa habari ni kwamba hali yake Sat-B ni nzuri kidogo.
kitu kinazidi kushangaza sana kwenye hii familia ya msanii Sat-b, nikwamba habari mbaya kila kukicha inawakabili sana uku mafanikio ikianza kuonekana basi na matatizo pia inajitokeza. Amepta fursa ya kwenda Kenya kujitangaza kimataifa uku akionekana kama msanii bora kati ya awo wasanii 10 wa Afrika mashariki akichukuwa na fasi ya 10. Baadae tu akiwa Kenya mwanamziki Sat-b amepata habari ya kwamba mtoto wake wa kwanza amepewa sumu, Mungu akafanza maajabu mtoto amepona na kwasasa eko na afya ya kuridhisha.
|
Mtoto wa Sat-b |
Ila baada tu kupata matatizo ya mtoto wake, naye ametekwa na kundi ya uko nchini Kenya ambao mpaka sasa awajajulikana na wakampora kila kitu. Baadae amefanya kama siku 3 familia na jamii nzima aijuwi mahali alipo uku akitia mioyo ya mashabiki na familia yake mashakani. Ila Mungu ameleta neema yake na mda siku mwanamziki Sat-b ameonekana na akawasili nchini Burundi mzima na afya nzuri.
|
Mdogo wake Sat-b, Bosingwa Radjabu |
Matatizo aikumalizika hapo baada ya ye msanii mwenyewe Sat-b kupata ajali ivi tena tumepata habari ya kwamba mdogo wake wa mwanamziki Satura nayeye amepewa sumu na yupo kwenye hali ambao sio nzuri kabisa. Mdogo wake ambae anajulikana kwa jina la Radjabu Bosingwa ambae amewahi kuichezea klabu ya Vital'o Fc akitokea kwenye klabu ya Maniema Fc, Bosingwa amepewa sumu na uku mkubwa wake pia Sat-b amepatwa na ajali, yaani kwenye familia ya Kalume kila kukicha ni matatizo mpaka sasa awajuwi kama kweli ni mipango wa Mungu ao ni mambo ya binadamu wasio kuwa na huruma.
Tuzidi kuwaombea duwa familia ya mwanamziki Sat-B Satura Amabafle, Mungu alete usalama na amani pia na ulinzi wa hali ya juu.
Post a Comment