MISHE-BOY

Romanus Orjinta kafariki Dunia



Romanus Orjinta

Wakati imekuwa ni mda wa kuaga mwaka wa 2014, uku kifo cha baadhi ya wachezaji kama Ebossé na Meyiwa. mwaka wa 2015 imekuja na habari mbaya . Mchezaji  wa zamani wa Nigeria  beki Romanus Orjinta alikutwa amekufa nyumbani kwake katika Enugu. mwaka wa 2003 ameibuka Mshindi wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye klabu yake ya  Enyimba mwaka 2003.
beki wa miaka 33 alikutwa amekufa katika nyumba yake na mpaka sasa sababu ya kifo chake akijapatwa ufumbuzi uku uchunguzi ukiendelea kufanya kazi yake. nchi nzima ya Nigeria iko kwenye maombolezo.
Senzo Meyiwa
2014 ulikua pia mwaka wa huzuni kwa wapenzi wa soka nchini Afrika Kusini baada ya kuuawa kwa nahodha wa Bafana Bafana kipa Senzo Meyiwa.
Mwezi Oktoba, Meyiwa alipigwa risasi na watu waliojihami kwa silaha jijini Johannersburg akiwa na mpenzi wake.Meyiwa aliisaidia Afrika Kusini kufuzu katika michuano ya Mataifa bingwa mwaka huu nchini Equitorial Guinea.
Albert Ebossé
Mbali na Meyiwa, kifo cha mchezaji mwingine kilichogusa wapenzi wa soka ni mchezaji wa klabu ya JS Kabylie ya Algeria, Mcameroon Albert Ebossé aliyepigiwa na kitu kizito kichwani na mashabiki wa wa JS Kabylie, baada ya klabu hiyo kupoteza mabao 2 kwa 1 dhidi ya USM Alger.
Albert Ebossé
Albert Ebossé


Hakuna maoni