Mtandao wa kijamii wa Facebook inapata mpinzani mkubwa kwajina lake mahafu kama Anti-Facebook ila ni Ello
Mtandao wa kijamii wa Ello unapokea
maombi 31,000 ya watumiaji wanaotaka kujiunga kila saa moja hali ambayo
inaibua ushindani mkubwa kwa mtandao wa Facebook.
Muanzilishi wa mtandao huo Paul Budnitz ameiambia BBC kuwa wakati mtandao huo unaazishwa ulilenga watu kuhudumia marafiki 90 tu.Mtandao huu kwa mjibu wa muanzilishi umeanzishwa August mwaka huu ukiwa ambapo hauna gharama yoyote kwa mtumiaji iwe matangazo ama kulipia data.
Hata hivyo baadhi ya watumiaji wameubatiza kwa jina la Anti-Facebook mtandao huo, wakimaanisha kwamba ndiye mpinzani mkubwa wa Facebook.
Baadhi ya wataalam wa masuala ya kimitandao wamekosoa mfumo wa Ello kutotoza gharama yoyote wakidai kuwa katika siku za usoni huenda mtandao wa Ello utalazimika kutoza kiasi kidogo cha fedha kwa watumiaji wake.
Paul Budnitz mtengenezaji wa baiskel za kampuni ya Vermont ameiambia BBC kuwa wapo imara katika ushindani wa kimitandao na kujigamba kuwa ana wataalamu wa kutosha kukabiliana na makampuni pinzania.
Hata hivyo kuhusiana na baadhi ya watu kuuiita kwa jinala bandia la anti-Facebook mtandao huo yeye amesema wanajiendesha kama mtandao wenye mtazamo wake binafsi na si kutegemea mtazamo wa mtandao wa Facebook.
Paul Budnitz |
Post a Comment