MISHE-BOY

ratiba kanuni la kombe ya CECAFA KAGAME CUP 2014

kombe ya Cecafa Kagame Cup ya huu mwaka itahanza ivi karibuni Kigali Rwanda, kwa habari kutoka hapa Burundi ni kwamba, klabu mbili ndizo itakao wakilisha Burundi kwenye kombe la Cecafa 2014, ni pamoja na Vital'o Fc ambao wanao shikilia kombe hio, na Atletico. kwakawaida nafasi ya Atletico ni klabu ya Flambeau ndio ingepashwa kwenda ila kunahabari inayo sema kwamba, baada ya uchunguzi kwenye shirikisho la FFB, wamegunduwa kwamba klabu ya Flambeau imekuwa inatowa rushwa kwenye baadhi ya mechi zake ili ipate na fasi ya kwanza kwenye ligi kuu ya Primus league. kwa madai hayo ndio sababu klabu ya Flambeau imeondolewa kwenye orodha ya kuwahakilisha Burundi kwenye kombe la Cecafa Kagame Cup 2014.
 pambano ya kwanza ya kufunguwa kombe hii ya CECAFA KAGAME CUP 2014, itahanza kwenye saa saba kamili (13h) Atlabara (Sud-Soudan) itapimana nguvu na klabu ya KMKM (Zanzibar), na mchezo wa pili saa tisa (15h) ni kati ya Rayon sports (Rwanda) dhidi ya  Azam (Tanzanie) ndio mechi ya kufunguwa kombe la CECAFA KAGAME CUP 2014 kwenye uwanja wa Amahoro na mchezo wa tatu ambao utakuwa wa mwisho siku ya kwanza la kombe hii ni kati ya Gor Mahia (Kenya) dhidi ya KCCA (Ouganda).

hapo tarehe 09/08/2014 ndipo klabu ya Burundi ya Vital'o inayo shikilia kombe hio, itacheza dhidi ya klabu kutoka Benadir (Somali) saa saba kamili (13h00').
saa tisa (15h00'), Police (Rwanda) dhidi El Merreikh (sud-Soudan), saa kumi na moja (17h00') APR (Rwanda) dhidi ya Atletic Olympic (Burundi).

tarehe 10/08/2014, kwenye uwanja wa Amahoro, KMKM (Tanzanie) dhidi Azam (Tanzanie).


tuwape historia fupi tu ya hii kombe la Cecafa cup, klabu ya Simba kutoka Tanzaania ndio inayo chukuwa na fasi ya kwanza kwa vikombe nyingi
  1. Simba Sports                         mara 6: 1974, 1991, 1992, 1995, 1996, 2002
  2. A.F.C. Leopards                  mara 5: 1979, 1982, 1983, 1984, 1997
  3. Young Africans                    mara 5: 1975, 1993, 1999, 2011, 2012
  4. Gor Mahia                           mara 5: 1976, 1977, 1980, 1981, 1985
  5. Tusker                                    mara 5: 1988, 1989, 2000, 2001, 2008
  6. Villa                                       mara 3: 1987, 2003, 2005
  7. Armée Patriotique Rwandaise mara 3:  2004, 2007, 2010
  8. Al-Merrikh                            mara1 :  1986
  9. Kampala City Council           1 : 1978
  10. ATRACO                               1 : 2009
  11. Uganda Police                        1 :2006
  12. Rayon Sports                         1 : 1998
  13. Vital’O                                    1 : 2013


tuwafahamishe kuwa CECAFA KAGAME CUP 2014, ni michuano ambao inakutanisha klabu 12 bingwa za Afrika ya kati na Afrika  mashariki, ambazo zimepangwa kwenye kundi 3.
Kundi  A
Kundi B
Groupe C
Young Africans (Tanzanie)
Ethiopia’Coffee (Ethiopie)
 Rayon Sports (Rwanda)
 Altabara (Soudan du Sud)
KMKM (Zanzibar)
Gor Mahia (Kenya)
APR FC (Rwanda)
Kampala City Council (Ouganda)
Atletico (Burundi)
Djibouti Telecom (Djibouti)
Vital’O (Burundi)
Sudan’s El Merreikh (Soudan)
Police (Rwanda)
Benadir (Somalie)

Hakuna maoni