MISHE-BOY

tizama wachezaji 19 warundi walio itwa,ni wachezaj wanao cheza mpira wa kulipa sehemu mbalimbali

timu ya taifa ya Burundi Intamba murugamba  hii ndio imeweka wazi orodha ya wachezaji wa kimataifa warundi wanao cheza mpira wakulipa ugenini na wanaitajiwa kwenye timu ya taifa ili kuandaa mechi ya kombe ya Can 2015 nchini Maroc. mechi ya kwanza watacheza na Botswana kati ya tarehe 16,17 na 18 April 2014, endapo wakifaulu kupita watajiunga kwenye kundi G ikiwemo  Misri , Tunusia na Senegal. hii hapa oradha kanuni ya wachezaji 19 waliitwa na nchi ya Burundi na kuna wachezaji mara yao ya kwanza kuitwa na Burundi kwa mchango mukubwa wa viongozi wapya wa mpira wa Burundi sanasana jitiada kubwa ya  Mheshimiwa Révérien, kuwaita wachezaji warundi ambao wamekuwa awana imani ya kuichezea nchi yao ila kwa ukaribu wa Mheshimiwa Révérien wamekubali na watakuja kujiunga na wenzao.
 hii ndio orodha kanuni ya wachezaji 19 walio itwa na Timu ya Taifa

1. NTIBAZONKIZA Saidi / Pologne
  kwa upande wa NTIBAZONKIZA Saidi yeye ni kawaida kuichezea timu yake ya taifa na jina mahafu mashabiki wanamuita ni Messi du Burundi (messi wa Burundi) amekwisha saidia sana nchi yake kisoka na mengine.

2. BERAHINO Saido  / Angleterre 
 kwa BERAHINO Saido  ni mara yake ya kwanza endapo atawasili hapa nchini kwamaana amekwisha onesha uwezo wakuja kuichezea nchi yake. na ni mchezaji wa Westbrom ya Uingereza.
 
3. BIGIRIMANA Gaël / Angleterre
kwa BIGIRIMANA Gaël   ni mara yake ya kwanza endapo atawasili hapa nchini kwamaana amekwisha onesha uwezo wakuja kuichezea nchi yake. na ni mchezaji wa Newcastle ya Uingereza.

4. NDIKUMANA Yamin Selemani /Albanie

 5.NAHAYO Valery / Belgique

6. HABARUGIRA David /Belgique

HABARUGIRA David  ni beki hatari wa FC Brussels na amewahai kupata mafunzo kwenye club ya Anderlech pamoja na beki mahafu wa Man city Kompany.









7.  KWIZERA Pierre / Côte d’Ivoire

8.Papy Faty  / Afrique du Sud

9.NSABIYUMVA Fréderic/ Afrique du Sud

10. NDUWARUGIRA Christophe / Mozambique

11. TAMBWE Amissi / Tanzanie

 12. KAVUMBAGU Didier / Tanzanie

13. KAZE Gilbert / Tanzanie

14. NIZIGIYIMANA Abdoul Karim / Rwanda

15. NDAYISENGA Fouadi / Rwanda

16. NIZEYIMANA Johane / Portugal

17. IRAKOZE Filose/ Suède

18.NZOKIRA Jeff / Djibouti
amefanya siku nyingi sana aitwi kwenye timu ya taifa Intamba Murugamba, ila kwa sasa kwa kipaji chake kudhiririka kwenye timu ya A.S.S. Djibouti Telecom kwa kuchukuwa kombe mara mbili na kupata zawadi ya golikipa bora misimu miwili na kwa sasa ni double man kwa jina maharufu nchini Djiboutie.ameitwa tena kwenye hii orodha ya huu mwaka na kufurahisha wapenzi wa soka mbalimbali ambao wamekuwa wanapiga kelele na kutaka wamuone kwenye timu ya taifa.

19. amissi Cedrick/ Rwanda

ukitizama listi hii, inatisha sana ki ivo na inatupa imani kubwa kwamba timu ya Taifa itaweza kufanya vizuri sana na kufika mbali endapo kocha akiwapanga vizuri na kupata mazowezi ya kutosha kwajili wazoweyane.
Burundi Fleva inaitakiya timu ya taifa kila la kheri.

Hakuna maoni