MISHE-BOY

ARSENE Wenger ametoa kali ya mwaka

kocha wa klabu ya Arsenal ya Ungerezan Arsene Wenger, ametoa kali ya Mwaka baada ya kudai kwamba alifahamu mchezaji mpya waliyemsajili mwezi Januari, Kim Kallstrom ni mgonjwa na kwamba kwake si kitu muhimu sana hata kama atashindwa kucheza mechi yoyote Arsenal.

 Mchezaji huyo aligundulika kuvunjika mfupa wa mgongo, lakini kwa presha ya siku ya mwisho ya kufunga usajili, Wenger aliamua kufanya usajili wa kiungo huyo licha ya kwamba madaktari walimwambia kuwa ni mgonjwa.
Lakini, Wenger aliyepitisha usajili wake na juzi Jumapili alikiri kwamba ameamua kumnasa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 na atakuwa kikosini kwake hata kama hatacheza mechi yoyote Arsenal hadi mwisho wa msimu.
 Kallstrom atakakuwa nje ya uwanja kwa kipindi ambacho kinatajwa kuwa ni wiki sita, klabu yake ya zamani ya Spartak Moscow ndiyo itakayokuwa ikimlipa mshahara na baada ya hapo litakuwa jukumu la Arsenal.
 Wenger alisema: “Nina hakika kama umewahi kucheza mpira, lazima uliwahi kucheza huku sehemu moja ya mfupa ikiwa imevunjika kidogo. Huwezi kujijua. Mimi nililiwaza hilo lakini nilifikiria zaidi kumaliza dili. Hawa Spartak watamlipa mshahara wake kwa wiki sita, lakini matarajio yangu atakuwa nje kwa wiki nne hadi sita. Acha hili lipite tutajua mwisho wa msimu kama tulikuwa sahihi au tulikosea.”

Hakuna maoni