MISHE-BOY

Sport : Aigle Noir, Kayanza United na Buja City zaanza vibaya Msimu 2019-2020

Aigle Noir C.S ya mkoani Makamba ambao ndiyo vinara wa ligi kuu Burundi, waaanza vibaya kwa kuchapwa na Les Lierres (1-2); kayanza United baada ya kusajili vizuri watambiwa na Flambeau du Centre (3-1) huku vijana wa Omar Ntakagero wakipigwa na LLB (1-2).

Ligi kuu Burundi ilianza kutimua vumbi wiki hii Agosti 10, 2019 katika viwanja tofauti.
Ikiwa uwanja wa nyumbani timu ya Olympic Star ya mkoani Muyinga ilikumbana na changamoto ya kufungwa mabao 2-1 kwenye mechi yake ya kwanza ya ligi kuu nchini Burundi ilipokutana na vijana wa kocha Djumaine, Musongati.

Aidha, timu ya Kayanza United licha ya kusajili sana waliridhika kutambiwa na Flambeau du Centre kwa mabao 3-1 wakiwa ugenini katika uwanja wa mkoani Gitega, Ingoma.
Buja City ilishindwa kujinusuru dhidi ya timu ambao ilinusurika kushuka daraja msimu uliyopita, Lydia Ludic Academic kwa kufungwa mabao 2-1.
Baada ya kutoka sare na Goh Mahia katika mchezo wa kwanza ya Ligi ya Mabingwa CAF, timu ya Aigle Noir ambao ndiyo   ilionekana wakisua sua mbele ya Les Lierres ikijikuta ikichezea kichapo cha mabao 2-1. 
Vijana wa Joslin Bipfubusa walipambana sana kujaribu kusawazisha bao hilo tangu hapo, lakini watoto wa mama Les Lierres walisimama imara kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu.

Matokeo ya mengine ya wiki ya kwanza ya Ligi Kuu Burundi, inter Star ilikwenda sare ya bila bila na messager Ngozi, Atletico Academy ikiitambia Messager Ngozi kwa mabao manne kwa bila (4-0) na Burundi Sport Dynamique ikipoteza pointi tatu kwa kupigwa bao moja na Bumamuru (0-1), hatimaye Rukinzo itakabiliana na Vital'o mwishoni mwa wiki hii.



Maoni 1

Bila jina alisema ...

The Emperor Casino - Shootercasino
If you are new to the gambling world and want to take a spin on some of the casino games of 2021, 메리트카지노 you should 제왕카지노 know what our expert febcasino team have here.