MISHE-BOY

Sport : Makenze Atangaza Kustaafu Kucheza Soka

Nahodha wa zamani wa kimataifa wa Burundi, Nizigiyimana Abdoul Karim maarufu Makenze ametangaza rasmi kustaafu kuchezea timu ya taifa Intamba Murugamba baada ya kudumu miaka 10 na kuchangia kuipeleka nchi yake kwenye Kombe la Afrika CAN2019 kwa mara ya kwanza katika historia.


Beki wa kulia  mwenye umri wa miaka 30, Karim amefikia maamuzi hayo baada ya kuichezea nchi yake kwa muda mrefu na sasa anaamini inatosha.

Makenz  hadi anatangaza kustaafu anaendelea kucheza katika vilabu pekee, kwasasa amechezea vilabu zaidi ya 7 ikiwemo Vital'o, A.P.R, Vipers, Kiyovu, Vita Club, Rayon Sport, Gor Mahia, ...

Kama hufahamu Makenze alizaliwa mwaka 1989 Juni 21 mkoani Kayanza nchini Burundi na alianza kucheza soka mkoani huko akaja kutambulika zaidi katika timu ya Vital'o mjini Bujumbura mwaka 2006 kwa jina halisi Nizigiyimana Karim lakini aliitwa Makenze kutokana na kiwango chake pia na  umbo mdogo kuliko wote katika timu ya vijana aliyokuwa anacheza wakati huo akiwa na umri mdogo.

Makenze alianza kuitwa katika timu ya taifa ya Burundi mwaka 2007, hiyo ni baada ya kufanikiwa kuipatia ubingwa timu yake ya Vital'o, hivyo nyota yake ya kuja kuwa staa wengi walianza kuiona mapema.

Kwa niaba ya Mishe Mishe, Makenze daima utabaki mfano katika timu ya taifa ya Burundi na Mungu atakulipa kwa mazuri ulioyafanyia nchi yako.

Hakuna maoni