Sport | Yaya Toure aondoka rasmi ndani ya Man City, Pep athibitisha
Katika mkutano na waandishi wa habari Ijumaa hii, Pep Guardiola alitangaza kuondoka kwa Yaya Toure mwishoni mwa msimu. Kocha wa Mancherster City pia alisema Sergio Aguero ambaye alifanyiwa upasuaji wa goti atakuwa tayari kwa Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.
Baada ya miaka nane na Man City, Yaya Toure(34) ataondoka klabuni mwishoni mwa msimu, aliwasili mwaka 2010 akitokea Barcelona, ambako alishinda kuelewana na kocha Guardiola.
Katika klabu ya Man City, Toure yaya ameshinda kombe tatu ya Ligi ya England ( 2012, 2014 na 2018) na kombe la FA mwaka 2011 na Cups League (2014, 2016, 2018).
Yaya Toure alicheza mechi 16 katika mahindano yote mnamo mwaka 2017-2018, lakini kocha wake anataka kumpa nafasi ya kwenda sehemu nyingine.
''Dhidi ya Brighton( mchezo wa mwisho), tutafanya kila kitu kushinda kwa kumpa shukrani kwa yote aliyosaidia timu.'' alisema Pep Guadiola.
Post a Comment