MISHE-BOY

News | Hawa aliyekuwa mke wa Mugisha kujiunga na Nuuru Salaam

Habari ya mjini kwa sasa ni kuwa aliyekuwa  mke wa kwanza wa muigizaji pia muimbaji wa nyimbo za kaswida nchini maarufu kwa jina la Mugisha, Hawa yupo mbioni kutia wino (kusaini) ndani ya Kundi Nuuru Salaam.

Mwanadada Hawa mwenye sauti inayo mtoa nyoka pangoni ambaye pia aliwai kuimba kaswida na aliyekuwa mmewe yuko mbioni kujiunga na kundi la Kaswida Nuuru Salaam na atakuwa msichana wa nne katika kundi hilo.
Nuuru Salaam
Habari hii imefichuliwa na mtu wa karibu wa Hawa na kusema kwamba kila mara anapenda kuizungumzia Nuuru Salaam na anapendelea  kuwa mwana Nuuru Salaam.

Baada ya uchunguzi tumegundua na kunasa video akionekana anajirikodi akikariri kaswida mpya ya Nuuru Salaam ikifahamika kwajila la Ya Nabi Salam Alayka na baadae akaipost kwenye Whatsapp yak (Status).

Wadau mnaonaje wazo la Hawa kujiunga na Nuuru Salaam, je kuna lolote litaongezeka kwa Kundi au kwa kuleta changamoto fulani kati yake na Mugisha?

Hakuna maoni