News | Bozi Boziana Kufanya Show nchini Burundi
Mwanamuziki wa Jamuhuru ya Kidemokrasia ya Congo, Bozi Boziana ametambulishwa jana na Zion Beach ikishirikiana na Bank ya BBCI mbele ya waandishi wa habari nchini Burundi kutumbuiza kwenye Concert VIP atashirikiana na wasanii kama Mike & Mimi, Rally Joe, Peace & Love pamoja na mchekeshaji maarufu nchini Kigingi.
Kwa mjibu wa tangazo la Concert hiyo, show imepangwa rasmi tarehe 12, Mei 2018 saa kumi na mbili (18h') kwenye ukumbi wa Zion Beach jijini Bujumbura.
Nguli huyo wa rumba aliwataka watu wote wanaopenda muziki huwo na mashabiki wa muziki wa kizazi kipya waje kwa wimbi siku hiyo wafurahi pamoja.
Post a Comment