King Touch : Big Fizzo wasasa anabebwa sio kama wazamani
Msanii wa muziki nchini Burundi anaendeleza kazi ya muziki nchini Afrika Kusini, King Touch ameonesha wazi ni miongoni mwa watu wanaompinga nyota wa Burundi, Big Fizzo.
Hitmaker wa wimbo NISHIKE MKONO, amemdiss wazi wazi kwenye kipindi cha BujaMusic (NickoJunior/online) na kusema kwamba wasanii wengi wanabebwa tu kwasababu tayari wamekwisha jenga jina ila ukitazama nyimbo yao kwasasa ni mbovu hautamani ku replay.
King Touch anadai Big Fizzo anabebwa na kudai ni suala ambalo lipo wazi kwa kuwa nyimbo zake za sasa hazina tena uzito kama za zamani.
Najua Big Fizzo ni msanii mkongwe ila kwa sasa media hasa zile zina wa watangazaji wachaga wanazidi kualazimisha na kuwaaminisha mashabiki kuwa big fizzo bado mkali kuliko wengine kitu ambacho sio kweli kabisa, kwa njia hiyo big fizzo ana hit wakati anaimba ujinga wakati wasanii kama Master Land, A Flow, Chris Bizz ata mimi na Tofy Gas tunatoa nyimbo kali zinabaniwa, alisema King Touch.
Post a Comment