Sport | Rukinzo FC yapanda daraja la kwanza Ligi Kuu Burundi
Rukinzo FC ya Bujumbura imekuwa timu ya kwanza kujihakikishia nafasi ya kupanda daraja Primus League nchini Burundi msimu ujao baada ya kuitambia wababe wao Dinamique FC kwa ushindi wa mabao 4-1 katika mchezo wa jana Jumapili, 29, Aprili.
Pointi tatu walioipata iliwatosha kabisa kuwa miongoni mwa timu zitakazi pambana Ligi Kuu Primus league msimu ujao kwa kusaka ubingwa daraja la kwanza.
Rukinzo FC imevuna jumla ya pointi 28 ambazo hazitafikiwa na klabu nyingine katika ligi hio ya daraja ya pili katika mechi 2 za mwisho zilizobaki ambapo kwa upande wa Transport , Dinamique na Muzinga ata Bumamuru wanafuata.
Aidha ushindi huo umekuwa ni heshima pekee kwa kocha mkuu wa timu hiyo Kocha Rama ambaye alikabidhiwa timu msimuu huu na moja kwa moja anatimiza ahadi yake.
Hii imekuwa mara ya kwanza kwa Rukinzo kushiriki Ligi ya Juu zaidi nchini Burundi, zaidi ya misimu miwili Rukinzo ilijitahidi kupanda daraja lakini ilijikuta kila mara ikishindwa, lakini msimu huu imekuwa ya mafanikio kwa klabu hiyo baada ya kupata kocha mpya ambaye aliwahi kuwa kocha wa timu kadhaa nchini Burundi.
Post a Comment