Sport | Mario Baloteli : Kama ningekuwa mzungu, singekuwa na matatizo mengi!
Mshambuliaji wa Italia ambaye alicheza baadhi ya timu nyingi kubwa kubwa, Inter Milan, AC Milan, Manchester City na Liverpool kwasasa akiwa Ufaransa katika timu ya Nice, Baloteli anadhani kama angekuwa mzungu (mweupe), angekuwa na matatizo madogo huko Europa.
Hata hivyo, mambo yake inazidi kuharibika na utata, alikiri kuwa ingawa anafanya baadhi ya matatizo na vituko vyake mwenyewe na kuzidi kupata adhabu kali, anaamini angeweza kusamehewa haraka zaidi kama angelikuwa mzungu au mtu mweupe.
'' Katika baadhi ya viwanja, watu mara nyingi walikuwa wanaimba kwa sauti kama hakuna Black mwenye asili ya Italia, lakini nina ushahidi kwamba kuna black mwenye asili ya Italia na ndio mimi.'' aliiambia Sofoot kupitia Mirros.al.
Baloteli aliongeza :'' ingawa mimi ni Muitaliano, nilizaliwa na kukulia nchini Italia, inasemekana kuwa nilipata uraia wakati nilikuwa na umri wa miaka 18. sheria ni uongo na labda ni kwanini baadhi ya watu leo wanaona rangi nyeusi kama rangi ya upungufu. Nadhani ningekuwa na rangi nyeupe ningekuwa nasamehewa haraka zaidi ila kwasasa tatizo yangu ndogo napata adhabu kubwa.''
Post a Comment